Short note: This website is in Beta - we are currently building everything up but you can already find the apps to download and participate! Thank you and stay safe!

Nini kinapaswa kuwa kwenye picha?

Hii inategemea aina ya kituo unachotaka kuripoti: kituo cha hali ya hewa, kituo cha maji, Hali ya Hewa@Nyumbani au Dokezo Picha.

Tazama maagizo ya kila aina ya kituo hapa chini:

1.) Je, uko kwenye kituo cha hali ya hewa?

Je, uko kwenye kituo cha hali ya hewa? Piga picha ya ubao wa taarifa. Hakikisha kwamba inawezekana kusoma namba kwenye kipima joto, kipima unyevunyevu na kipima mvua kutoka kwenye picha (angalia mfano hapa chini).

ID 1669 water station

2.) Je, uko kwenye kituo cha maji?

Piga picha ya kipima(rula) kiwango cha maji kwenye maji (tazama mfano hapa chini) na uhakikishe kuwa inawezekana kusoma namba za kiwango cha maji kutoka kwenye picha. Kumbuka kwamba kipimo cha kiwango cha maji kwenye kituo chako kinaweza kuonekana tofauti kidogo kuliko katika mfano.

ID 1669 water station

3.) Je, ungependa kuripoti kutoka kwa kituo chako cha Hali ya Hewa@Nyumbani?

Piga picha ya kipimo chako cha mvua (tazama mfano hapa chini) na uhakikishe kuwa inawezekana kusoma thamani za namba kwa urahisi.

ID 1669 weaterhome

4.) Je, ungependa kuripoti dokezo picha?

Hizi zinaweza kutumika kushirikisha picha za aina yoyote ya matukio ya hali ya hewa, kwa mfano dhoruba ya mvua ya mawe, mafuriko au mto mkavu. Hapa kuna baadhi ya mifano:

ID 1669 photo note flood

Kwenye picha hapo juu unaweza kuona mto uliofurika.

ID_1669_photo_note_dry_river.jpg

Kwenye picha hapo juu unaweza kuona mto unakaribia kukauka.

ID 1669 photo note soil erosion

Kwenye picha hapo juu unaweza kuona mmomonyoko mkubwa wa udongo (mvua imeondoa sehemu ya udongo).

ID 1669 photo note drought 1

Kwenye picha hapo juu unaweza kuona ukame.